DEREVA MWINGINE ANUSURIKA KIFO FORMULA 3 NCHINI ITALIA
Wiki moja baada ya kupata pigo kwa kumpoteza dereva Anthoine Huberth wa Formula 2, wikiendi hii ililazimika mazoezi ya mbio za Italian Grand Prix za formula 1 kuchelewa kuanza baada ya ajali mbaya kutokea katika formula 3 huko Italia.
Dereva Alex Peroni wa Formula 3 alipata ajali mbaya katika Italian Grand Prix baada ya gari lake kugonga kizuizi na kuruka hewani likizunguka mara 3 kabla ya kutua chini.
Mashabiki na wasimamizi wakiwa katika hamaki dereva Alex Peroni alitoka katika gari akiwa salama bila mchubuko wowote na kuchukuliwa pelekwa hospitalini kwa ajili ya uangalizi.
Wakati huo huo Dereva Juan Manuel Correa aliyekuwepo katika ajali iliyomuua Anthoine Hubert nchini Ubelgiji wiki iliyopita, yupo anaendelea na uangalizi wa matibabu akiwa katika comma katika Hospitali moja jijini London.