LOUS VAN GAAL ATUA RWANDA KWA AJILI YA KWITA IZINA
Utalii ni sekta ambayo huingiza fedha nyingi za kigeni nchini Rwanda. Inaelezwa kuwa, utalii wa sokwe wa milimani ni chanzo namba moja cha fedha za kigeni nchi humo.
Kila mwaka nchini Rwanda hufanyika sherehe kubwa ya kuwapa majina watoto wapya wa sokwe.
sherehe hiyo maarufu kwa jina la “Kwita Izina”, huhudhuriwa na watu mashuhuri lufufu kutoka sehemu mbalimbali.

Kocha wa zamani wa Man United Mholanzi Louis Van Gaal, ni moja ya watu ambao wamefika nchini Rwanda kwa ajili ya sherehe hizo.
Nahodha wa zamani wa Arsenal Tony Adams nae anatarajiwa kuwepo, mwanamziki Ne-Yo kutoka Marekani,mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell nao ni moja ya watu mashuhuri watakaokuwepo.

Watoto 25 wa sokwe waliozaliwa kati ya Septemba 2018 na Septemba 2019, wanatarajiwa kupewa majina leo Septemba 6 katika sherehe hizo ambazo zimekuwa maarufu tangu mwaka 2005.