NADAL ATINGA NUSU FAINALI US OPEN 2019
Michuano ya US Open ikiendelea shika kasi katika viunga vya Flushing Meadows, mchezaji namba 2 kwa ubora duniani Rafael Nadal amefanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali baada ya kumfunga Diego Schwartzman kwa seti 6-4, 7-5, 6-2 katika mchezo wa robo fainali.
Nadal sasa atakutana na Muitalia Matteo Berrettini aliyefuzu hatua ya nusu fainali kwa kumtoa Gael Monfils robo fainali.
Kwa upande wa wanaume, tofauti na Nadal wachezaji wengine wote watatu Berrettini, Grigor Dimitrov na Daniil Medvedev hawajawahi kufika hatua ya fainali katika Grand Slam.
Sasa Nadal atakuwa na nafasi ya kuisogelea rekodi ya Federer mwenye Grand Slam 20 kwa kuwa nyuma ya Grand Slam moja endapo atatwaa ubingwa huu wa US Open.