XENOPHOBIA YAMKIMBIZA STAA WA SOKA WA TANZANIA AFRIKA KUSINI NA KUJIUNGA NA FC LUPOPO
Mchezaji wa kitanzania Uhuru Seleman ameamua kuondoka klabu ya Royal Eagles ya Daraja la kwanza ya Afrika Kusini na kujiunga na FC Lupopo ya Ligi Kuu ya Congo kwa kandarasi ya miaka miwili.

Uhuru amesema kuwa amefikia maamuzi hayo kufuatia kuchoka kukaa mbali na familia yake na pia kuchoshwa na ubaguzi wa wageni (Xenophobia) unaoendelea nchini Afrika Kusini.
Kufuatia machafuko na ubaguzi huo, mchezaji huyo wa zamani wa Simba ameshindwa kuishi pamoja na familia yake nchi Afrika kusini, hivyo sasa amefikia maamuzi ya kuondoka.
.
“Sababu kubwa ya kuondoka ni kutokana na ubaguzi na machafuko ambayo hayaishi, kila siku tunapata vitisho, haviishi.” amesema Uhuru.
