PEP GUARDIOLA AJIUNGA NA GIRONA
Kocha Pep Guardiola amejiunga na klabu ya Girona ambayo ilishuka daraja kutoka ligi kuu nchini Hispania La Liga msimu uliopita.
Mhispania huyo hajajiunga na Girona kama kocha, amejiunga kama mwanachama wa klabu hiyo ambayo inamilikiwa na kuendeshwa na kaka yake ,Pere Guardiola.
Baada ya kupewa kadi yake ya uanachama hapo jana, Pep akiwa pamoja na kaka yake, alienda kuangalia mazoezi ya timu hiyo na baada kuongea na kocha wao Juan Carlos Unzue na wachezaji wa kikosi cha kwanza.