SERENA WILLIAMS AENDELEA PAMBANA KUIFIKIA REKODI YA MARGARET COURT
Katika mechi iliyoisha kwa ushimdi wa seti 6-3, 6-4 dhidi ya Petra Martic aliyepo katika nafasi ya 22 kwa ubora, Serena Williams, 37, alihitaji uangalizi wa matibabu katikati ya mechi ili kuweza maliza mechi hiyo baada ya kupata maumivi katika mguu.
Bingwa huyo mara 6 sasa atakutana na Mchina aliyepo katika nafasi ya 18 kwa ubora Wang Qiang katika robo fainali. Serena anahitaji shinda taji hili ili apate fikia rekodi ya Margaret Court ya kushinda grand slam 24.