BEGA LAMTOA NOVAK DJOKOVIC US OPEN 2019
Bingwa wa mtetezi wa US Open Novak Djokovic ametolewa katika michuano hiyo baada ya kuumia bega lake la kushoto katika mchezo wa raundi ya nne dhidi ya Stan Wawrinka.
Mpaka wakati huo Djokovic anaumia,Stan Wawrinka alikuwa akiongoza kwa seti 6-4,7-5,2-1.
Wawrinka,34,atacheza na Mrusi Daniil Medvedev katika hatua ya robo fainali.