Mitandao ya Ubelgiji imefikia hatua ya kumlinganisha Samatta na Lukaku
Mbwana Ally Samatta jina ambalo linatawala vichwa vya habari vya magazeti ya michezo Ligi Kuu Ubelgiji kufuatia uwezo ambao amekuwa akiendelea kuuonesha akiitumikia klabu yake ya KRC Genk ya nchini humo.
Kufuatia kipaji chake cha kipekee na uwezo wa kufunga kila leo Mbwana Samatta amefikia hatua ya kulinganishwa na mbelgiji anayecheza Manchester United Romelu Lukaka huku Samatta akitajwa bora zaidi ya huyo kulingana na uwezo wake wa msimu huu.
Moja kati ya ukurasa wa instagram mkubwa wa michezo unaoitwa KRCGENKMPVA wenye wafuasi zaidi ya laki moja, umewapost Samatta na Lukaku na kuanza kuwalinganisha kwa data na kusema Samatta ni bora kuliko Lukaku.
Samatta msimu huu ameichezea KRC Genk michezo 16 na amefunga magoli 13 na kutoa pasi mbili za usaidizi wa magoli wakati Lukaku akiwa na Manchester United amefunga magoli manne katika michezo 14 akiwa hajatoa pasi yoyote ya usaidizi wa goli, hivyo fan page ya KRCGENKMPVA ikamtaja Samatta ni bora kuliko Lukaku kama ambavyo baadhi ya watanzania huwa wanawakejeli mashabiki wa Manchester United kutokana na uwezo wa mchezaji huyo.