LECLERC ATWAA USHINDI WAKE WA KWANZA F1 NA KUUTOA KWA HESHIMA YA ANTHONIE
Baada ya kukaribia kushinda mbio za Bahrain na Austria na kupoteza katika mizunguko ya mwisho, wikiendi hii katika Belgium Grand Prix ilikuwa ni tofauti kwa Charles Leclerc, 21, aliyefanikiwa kuibuka na ushindi wake wa kwanza wa F1 mbele ya bingwa wa dunia mara 5 Lewis Hamilton. Nafasi ya tatu imeenda kwa Valtteri Bottas, Sebastian Vettel nafasi ya 4.

Ilitegemewa kuwa siku ya furaha kwa dereva huyu kijana wa timu ya Ferrari lakini haikuwa hivyo kwani ubingwa huu aliutoa kwa heshima ya dereva Anthonie Hubert wa Formula 2 aliyepoteza maisha hapo juzi kwenye ajali katika mbio.

Leclerc, Pierre Gasly pamoja na Anthonie Hubert walikuwa marafiki wa karibu ambapo wakiwa wamekuwa wote tokea wakiwa na miaka 7. Mbio hizi zitsendelea weekend ijayo katika Italian Grand Prix.