FORMULA 2 YAPATA PIGO BAADA YA DEREVA ANTHONIE HUBERT KUPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI
Mbio za Formula 2 zikiendelea katika Belgium Grand Prix weekend hii, zimepata pigo baada ya dereva Mfaransa Anthoine Hubert aliyekuwa na miaka 22 kupoteza maisha katika ajali iliyohusisha gari lake na la Mmarekani Juan Manuel Correa wakiwa katika mwendo wa 270km kwa saa (270km/h).
Chama cha mbio za magari FIA kilisema Hubert alipoteza maisha baada ya kufikishwa kituo cha afya na Correa alikimbizwa hospitalini na hali yake yaendelea vyema.

Mbio hizo zilisimama baada ya ajali hiyo na kuhairishwa kabisa baada ya taarifa rasmi juu ya Hubert kutoka muda mfupi baadae.
Formula 2 wamesema mbio za Jumapili hazitakuwepo kwa heshima ila mbio za formula 3 zitaendelea.
Hubert alikuwa akiendesha katika timu ya BWT Arden, na alikuwa akishika nafasi ya 8 katika msimamo wa madereva huku akiwa ameshinda mbio mbili za Monaco na Ufaransa.
Pia alikuwa katika program ya vijana madereva ya RenaultF1 young drivers programme ambapo alikuwa akishiriki formula 2 ikiwa ndio hatua ya mwisho kabla ya kuingia katika mbio za formula 1.

Timu ya Renault, Mercedes, timu nyingine, madereva wengi wa mbio hizo wakiwemo Ferdnando Alonso, Lewis Hamilton, Max Verstapen pamoja na wadau wengine wa mchezo huo kupitia taarifa rasmi na kupitia mitandaoni wameonyesha kusikitishwa sana na tukio hili.