Mauricio Pochettinho akataa kukata tamaa klabu bingwa Ulaya
Meneja Maurcio Pochettino wa Tottenham Hotspur anaamini timu yake inaweza kufuzu hatua ya mtoano kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya ushindi wa jana dhidi ya PSV.
Zikiwa zimebaki dakika 12 kwenye uwanja wa Wembley, Spurs walikuwa nyuma kwa goli moja. Magoli ya dakika ya 78 na 89 yaliyofungwa na Harry Kane yanaipa Spurs ushindi katika uwanja wao wa nyumbani.
Huo ulikuwa ni ushindi wao wa kwanza katika klabu bingwa msimu huu ambao unawaweka nafasi ya tatu katika kundi B,pointi tatu nyuma ya Inter Milan walio nafasi ya pili na mechi ijayo watakwenda Wembley.
“ Kama tunaweza kumfunga Inter hivyo wote tutakuwa na pointi saba “ amesema kocha huyo Muargentina.
“ Halafu kwenye mechi moja chochote kinaweza kutokea. Tutaenda Barcelona ( Kwa ajili ya mechi ya mwisho ya kundi ) kujaribu kushinda mechi. Imani bado ipo pale. Nina matumaini makubwa. “
Barcelona wao wamekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano hiyo msimu huu baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Inter Milan jana Giuseppe Meazza.
Barcelona wanaongoza kundi wakiwa na pointi 10 baada ya kushinda mechi zao tatu na sare moja, Inter Milan wakiwa nafasi ya pili na pointi 7 , huku vijana wa Pochettino wakishika nafasi ya na pointi nne, mkiani wapo PSV wenye pointi moja.