OSAKA AKOSHA MIOYO YA WATU AKIMPELEKA COCO GAUFF NYUMBANI
Kuanzia Kobe Bryant, Nicole Gibbs, Katie Boulter hadi Bellie Jean King na wapenda tenis wengine walishindwa kuficha hisia zao juu ya Naomi Osaka baada ya mechi yake ya ushindi wa 6-3, 6-0 dhidi ya kinda Coco Gauff na kumtoa katika mashindano ya US Open huku yeye akiendelea mbele raundi ya 4.

Punde baada ya ushindi wake Naomi Osaka,21,ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo alimwendea kinda huyo aliyekuwa akilia na kuanza kumfariji.
Katika mahojiano Coco Gauff,15, hakusita kusifia ukarimu huo akisema “Alikuwa akilia ameshinda. Nilikuwa nalia, kila mmoja alikuwa analia. Sikujua kwanini analia na nikashangaa sababu ameshinda”.
Kwa upande wa Osaka alimsifu Gauff kuwa moja ya wachezaji wanaokuzwa vyema na kuwa hakutaka amwache na maumivu hasa baada ya kukumbuka bado ni mdogo.

Kupitia mitandao ya kijamii wachezaji na wanamichezo wengine akiwemo mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu Kobe Bryant pamoja na wadau mbali mbali hawakusita mpongeza Osaka kwa ukarimu wake na kusema ameonyesha ukomavu na maana halisi ya michezo.