F1 KUENDELEA WEEKEND HII HUKU VALTTERI BOTTAS AKIBAKIZWA MERCEDES MSIMU 2020
Baada ya mapumziko mbio za F1 zinaendelea weekend hii sasa ikiwa ni Belgium Grand Prix dereva Lewis Hamilton akienda na uongozi wa point 62 mbele ya Bottas na ukiwa ni mwaka mmoja tokea Sebastian Vettel wa Ferrari kushinda mbio.

Bottas anaingia katika mbio hizi akiwa tayari amekamilisha makubaliano ya mkataba kubakia Mercedes mwaka 2020 na kumaliza sintofahamu za nani angeendesha timubmoja na mkali Lewis Hamilton. Sasa Mercedes wamemwachia dereva wao wa aiba Esteban Ocon kujiunga na Renault mwaka 2020.

Kibarua kitakuwepo kwa dereva mpya wa RedBull Alexander Albon ambae amejiunga katikati ya msimu huu kuchukua nafasi ya Pierre Gasly aliyeshindwa fanya vyema na timu hiyo. Sasa ana mbio 9 za kuonyesha uwezo wake ili kubakia katika timu hiyo pamoja na dereva Max Versttapen.

Dereva Kimi Raikonnen wa Alfa Romeo anaenda kwenye mbio hizi akiwa na jeraha la mguu baada ya kupata maumivu ya msuli ila hajakatatamaa na kudai bado anaweza shindana. Hali hii imefanya timu yake kumwita dereva wao wa akiba Marcus Ericksson na kumfanya kukosa mbio za IndyCar