CRISTIANO RONALDO AWEKA WAZI ANA MAHUSIANO MAZURI NA MESSI
Jijini Monaco Ufaransa usiku wa Agosti 29 2019 ilitolewa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya na waliokuwa wameandaa (UEFA), huku kwa mwaka huu ikiwa ina wananiwa na Lionel Messi wa Barcelona, Cristino Ronaldo wa Juventus na Virgil van Dijk wa Liverpool.
Van Dijk ndio ameibuka mshindi wa tuzo hiyo na kuwashinda vigogo Messi na Ronaldo.
Kabla ya kutolewa kwa tuzo hiyo Ronaldo alieleza juu ya uhusiano wake wake Lionel Messi akisema kuwa wako katika mahusiano mazuri na Messi huku akisifu kwa wote wawili kuwa bora kwa muda mrefu.
.
“Tumekuwa tukichangia jukwaa mimi na yeye (Messi) kwa miaka 15 ,sijui kama imewahi kutokea katika soka watu hao hao wawili kutawala katika jukwaa kwa muda wote huo sio rahisi, bila shaka tuna mahusiano mazuri lakini hatujawahi kula chakula cha jioni pamoja lakini kwa siku za baadae ninatumai litatokea.
nimemiss kucheza Hispania,mimi na yeye (Messi) tu tunashindana kwa miaka 15 , ananifanya ninafanya vizuri na ninamfanya afanye vizuri , vizuri tumekuwa sehemu ya historia ya soka” alisema Ronaldo wakati wa utolewaji wa tuzo hizo