USHINDI WA TUZO YA VAN DIJK WAANDIKA HISTORIA UEFA
Tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya ni tuzo ambayo ilianzishwa na UEFA mwaka 2011 kwa kushirikiana na vyombo vya habari za michezo vya Ulaya, ambapo hutolewa kwa wachezaji wanaocheza soka katika vilabu vya Ulaya.
Beki wa Liverpool Virgil Van Dijk ndio ameshinda tuzo hiyo kwa msimu wa 2018/2019 na kuandika rekodi ya kuwa beki pekee na wa kwanza kuwahi kushinda tuzo hiyo toka kuanzishwa kwake 2011.
Cristiano Ronaldo ndio mchezaji pekee aliyetwaa tuzo hiyo mara nyingi, amechukua mara tatu (2013/14, 2015/16 na 2016/17) mara mbili ikiwa mfululizo, Messi amewahi kuchukua mara mbili (2010/11 na 2014/15).