ATKINSON KUCHEZESHA MECHI YA ARSENAL NA TOTTENHAM
Ligi Kuu England imemtangaza mwamuzi Martin Atkinson kuwa ndio atakayechezesha mchezo wa Jumapili wa North London Derby unaozihusisha timu za Arsenal na Tottenham.
Timu hizo mbili zinakutana katika uwanja wa Emirates huku zote zikiwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo iliyopita, Arsenal akipoteza dhidi ya Liverpool 3-1 huku Tottenham akipoteza 1-0 dhidi ya Newcastle.
Mara ya mwisho refa Martin Atkinson kuchezesha North London Derby ilikuwa mwaka 2015 ambapo mchezo ulimalizika 1-1.