FC BARCELONA HAWAJAKATA TAMAA WANAKOMAA NA NEYMAR
Baada ya kikao cha takribani saa nne kati ya FC Barcelona na uongozi wa klabu ya Paris Saint Germain kuhusu usajili wa Neymar, FC Barcelona wametenga dau jipya tena mezani.
Mtandao wa daily mail umeripoti kuwa Barcelona sasa wameweka mezani ofa ya Pauni milioni 153 baada ya kukaa kikao hicho jijini Paris ili kumsajili Mbrazil huyo.
Upande wa Barcelona uliwakilishwa na Eric Abidal ambaye ni mkurugenzi wa soka wa timu na Oscar Grau ambaye ni Mkurugenzi mtendaji mkuu huku PSG wakiwakilishwa na Mkurugenzi wao mkuu wa michezo Leonardo na Meneja mkuu wao Jean-Claude Blanc.
Hata hivyo Barcelona bado inajishauri kuhusiana na ombi la PSG la kutaka pia wapewe Ousmane Dembele katika dili hilo,
Pia imeelezwa kuwa kikao hicho kinatajwa kuwepo na mvutano kwa sababu PSG hawajakubali ombi la Barcelona la kutaka malipo hayo yafanyike kwa awamu mbili.
Tukukumbushe tu Neymar alijiunga na PSG 2017 akitokea FC Barcelona kwa uhamisho wa rekodi ya dunia unayotajwa kufikia kiasi cha Pauni milioni 200.