PIQUE NA VIDAL WAIBUKA WASHINDI NA KUVUTA MTONYO.
Mwenye nacho huongezewa. Wachezaji wa FC Barcelona Arturo Vidal na Gerrard Pique wamebahatika kuibuka washindi wa European Poker Tour Event na kushinda kiasi kinachotajwa kufikia euro 500000 zaidi ya Tsh Bilioni 1.2.
Katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumatatu hii huko Barcelona, Pique amemaliza nafasi ya pili na kushinda kiasi cha euro 352,950 ambazo ni sawa na Tsh milioni 900 wakati Vidal aliyeshika nafasi ya tano ameshinda euro 134460 zaidi ya Tsh milioni 340.
Poker ni mchezo wa kadi ambao mara nyingi huwa unachezwa Casino ukihusisha Kamari,mbinu na ujuzi.
Hii si mara ya kwanza wachezaji wa Barcelona kushiriki katika mchezo huo, mwaka 2016 Neymar Jr akiwa katika timu hiyo, aliwahi kushinda Dola 10,000 (Tsh Milioni 22) katika mashindano ya Poker huko Las Vegas,Marekani.