ARSENAL WALISHAFUNGWA KWENYE REKODI YA BIG SIX, LIVERPOOL WAMEKAMILISHA TU!!
Mchezo wa Arsenal dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield ulichezwa huku wengi wakiwa na shauku ya kutaka kufahamu ni timu ipi itakuwa mbabe wa mwenzake katika Ligi Kuu England wakati huu ikiwa mbichi.
Arsenal kaendelea kuwa mteja wa vilabu vya Big Six akicheza ugenini baada ya Liverpool kuwaadhibu kwa mabao 3-1, mabao yakiwekwa wavuni na Joel Matip dakika ya 31 kwa kichwa, MO Salah akipachika mawili kwa penati dakika ya 49 na 58 huku Lucas Torreira akiwafuta machozi mashabiki wa Arsenal kwa kufunga bao dakika ya 85.
Kama hufahamu katika ligi rekodi toka 2015 huwa hazimbebi Arsenal dhidi ya timu sita kubwa Ligi Kuu England (Big Six) akicheza ugenini toka 2015 akiwa hajawahi kushinda katika michezo yote 23, sare zikiwa 8 na kupoteza mara 15.
Sasa Arsenal amefikisha jumla ya siku 1679 bila kuwafunga vigogo wa Big Six akicheza ugenini toka 2015 katika ligi kuu.
Big Six ni timu sita za EPL ambazo mara nyingi humaliza nafasi sita za juu ambazo ni Arsenal, Chelsea, Liverpool, Man United, Man City na Tottenham Hotspurs.