LIONEL MESSI AMESAINI LIGI DARAJA LA TATU NORWAY
Lionel Messi amejiunga na Klabu ya IK Junkeren ya Kaskazini mwa Norway inayoshiriki Ligi daraja la tatu. Ndio, umesoma sahihi, ni Lionel Messi.
Kijana Daniel Are Knutsen ,16, aliyeamua kubadili jina lake na kujiita Lionel Messi ikiwa ni heshima kwa mchezaji huyo ambaye anamhusudu kwa muda mrefu, amesajiliwa na timu hiyo ya daraja la tatu huko nchini Norway.
Daniel Are Knutsen (Messi) ameweka wazi kuwa kutokana na kumpenda Messi amekuwa akiiga vitu mbalimbali vya nyota huyo ikiwemo aina ya uchezaji na utambulisho wake.
.
“Nimekuwa na mpango wa kubadili jina langu kwa muda mrefu na Lionel Messi ndio role model wangu, kwa malengo yangu katika soka hakuna kitu kizuri kuliko kujaribu, ninataka kusema kuwa ninataka kujaribu kadri ya uwezo wangu kucheza kama yeye” alisema Daniel Are Knutsen (Messi) akihojiwa na gazeti la Norway VG
Daniel alikiri kuwa kipaji chake hakipo karibu hata kidogo na Lionel Messi lakini anajaribu kila kitu na kumuiga pindi awapo uwanjani.