Mchezaji auliwa baada ya kukutwa na mke wa mtu.
Mke wa mtu ni sumu. Mchezaji wa Brazil Daniel Correa anayeicheza klabu ya Sao Bento kwa mkopo kutoka Sao Paolo amekutwa amefariki porini koo lake na sehemu za siri zikiwa zimekatwa huko Sao Jose dos Pinhais nchini Brazil baada ya kukutwa kitandani na mke wa mtu.
Kiungo huyo,24, alienda kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa mwanadada mmoja anayefahamika kwa jina la Allana ambaye alikuwa anatimiza umri wa miaka 18. Sherehe zilianza klabu usiku wa Oktoba 26 na kuendelea nyumbani kwa wazazi wa mwanadada huyo.
Picha mbalimbali zimevuja zikimuonesha Correa akiwa kitandani na mama yake Allana, mwanamama huyo akiwa amevaa nguo ile ile aliyoivaa kwa sherehe.
Picha hizo zimetoka kwenye meseji za WhatsApp za Correa alizowatumia rafiki zake katika nyakati zake za mwisho.
Kwenye meseji moja alijitapa : “ Ninaweza kulala hapa. Kuna wanawake wengi wanalala kwa hii nyumba.” Nyingine ilisomeka : “ Ninaenda kumla mama wa Birthday girl …na baba yake akiwa hapa “
Rafiki yake mmoja akamjibu kwa kumkanya : “ (Mume wake) kalala ? Hakuna kitu utaweza kufanya,watakupiga na kukutoa nje ya nyumba.
“Watakuja kukusaga saga , huyo jamaa atakuja na kukupiga “ aliongeza mwingine.
Polisi wanaamini kuwa Daniel alipigwa na kuuliwa katika nyumba hiyo na mwili wake kuchukuliwa ndani ya gari na kutupwa porini.
Sehemu zake za siri zilitolewa baada ya kufariki. Maafisa wa polisi hawana hakika kama mchezaji huyo alifanya mapenzi na mama huyo, Cristiana.

Siku tatu baada ya tukio hilo, mume wa Cristiana, Edinson Brittes,38, alikamatwa na polisi na kukiri kuwa alimuua mchezaji huyo akiwa na hasira.
Edson anasema kuwa aliamua kuvunja mlango wa chumba chake baada ya kukuta umefungwa huku mkewe akiwa anapiga kelele ndani.
Alisema : “ Nilivyomvuta mke wangu , nikamrusha chini (Correa) kumzuia yule mzimu asimbake mke wangu.
Nilimpiga sana, sana na kumtoa nje ya nyumba. Sikujua alikuwa macho au kapoteza fahamu au alikuwa kafumba macho tu “
“ Hakuna nilichokuwa ninafikiria. Nilikuwa nina kisu kwenye gari langu,kisu kidogo. Sikujua nilikuwa ninaenda kufanya vile. Nilikuwa mwenye hasira na ghadhabu. “
Polisi wamewatia mikononi pia mke wa Edson na mwanae wa kike, wakituhumiwa kujaribu kuficha ushahidi wa mauaji.