KMC WAMEANGUSHWA NA UGENI, AS KIGALI WAKAWAMALIZA TAIFA
Kwa mara ya kwanza Tanzania imepata ushiriki wa vilabu vinne katika michuano ya kimataifa kwa msimu mmoja (2019/20) kwa mashindano yanayoandaliwa na shirikisho la soka Afrika (CAF).
KMC inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni ilikuwa ni miongoni mwa timu hizo nne yenyewe ikishiriki michuano ya Kombe la shirikisho Afrika na kutolewa na AS Kigali ya Rwanda kwa ushindi wa jumla ya 2-1 baada ya mchezo wa kwanza Kigali kuisha 0-0.
Hivyo KMC ikaaga mashindano hayo kwenye ardhi ya nyumbani, kocha msaidizi wa KMC Mlage Kabange amesema kuwa uoga ndio umewagharimu na baadhi ya wachezaji wake kama Boniface Maganga kushindwa kucheza vizuri kutokana na kuwa wageni katika mashindano hayo.