USAJILI WA DAKIKA YA MWISHO WAIBEBA AZAM FC DHIDI YA FASIL KENEMA
Klabu ya Azam FC imeendeleza rekodi yake ya kuhakikisha hakuna mgeni wa mechi za kimataifa atakayetoka Chamazi akiwa ana tabasamu zaidi ya kuondoka kichwa chini.
Azam FC ambayo mchezo wa kwanza dhidi ya Fasil Kenema ya nchini Ethiopia kupoteza 1-0, jana imepindua matokeo na kuitoa Fasil Kenema kwa kuifunga mabao 3-1, na hivyo kupita kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2.
Mabao mawili yalifungwa na Richard Djodi ambaye ndiye mchezaji wa mwisho wa Azam FC kusajiliwa msimu huu.
Obrey Chirwa dakika 58 alifunga goli la ushindi baada ya Fasil Kenema kupata bao moja dakika ya 37 kupitia kwa Mujibu Kassim.
Baada ya kupita raundi ya awali Azam FC atacheza dhidi ya Tringle FC ya Zimbabwe katika raundi kwanza.
Triangle wameitoa Rukinzo FC ya Burundi kwa idadi ya jumla ya mabao 5-0, baada ya jana mchezo wao wa marudiano nchini Burundi kumalizika 0-0.
Mchezo wa kwanza wa Azam FC dhidi ya Triangle FC utachezwa kati ya Septemba 13-15 2019 Azam akianzia nyumbani na marudiano kati ya 27-29 2019.