KLABU YA LIVERPOOL IMETANGAZA KUREFUSHA MKATABA WA CHAMBERLAIN
Liverpool wamethibitisha kuwa wameamua kumuongezea mkataba winga wao Alex Oxlade Chamberlain hadi mwaka 2023, hiyo ni baada ya kuridhishwa na kurejea kwake akitokea majeruhi.
Chambarlain ,26, alikuwa nje ya uwanja toka Aprili 2018 baada ya kuumia goti lakini alirudi vizuri mwishoni mwa msimu uliomalizika.
Tukukumbushe tu Chamberlain alijiunga na Liverpool 2017 akitokea Arsenal kwa dau la pauni milioni 35, hadi sasa akiwa kawafungia mabao matano katika michezo 47 aliyoichezea Liverpool.