ANDERLECHT YAMUONDOA KOMPANY UKOCHA KUELEKEA MECHI NA SAMATTA
Baada ya klabu ya Anderlecht kuwa na mwanzo mbaya wa msimu ikiwa ni mara ya kwanza kuwa na mwanzo huo mbaya ndani ya miaka 21, uongozi wa klabu hiyo umemuondoa Vincent Kompany ,33, kama kocha mchezaji katika siku za mechi.
Kompany akiwa kocha mchezaji klabu hiyo katika michezo minne ya mwanzo wa ligi msimu huu,imechukua pointi mbili baada ya kufungwa mechi mbili na sare mechi mbili.
Timu hiyo sasa imetangaza Kompany atabakiwa kuwa nahodha wa tu katika siku za mechi, na majukumu ya ukocha yote atakuwa akiyafanya kocha mkuu Simon Davies.
Katika mkutano wa waandishi wa habari leo, Davis amesema mabadiliko hayo yatafanya Kompany kuwa na umakini zaidi katika kucheza katika siku za mechi.
Mabadiliko hayo yataanza rasmi kesho kwenye mchezo dhidi ya KRC Genk utakaochezwa saa 3:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki