JUNIOR AGOGO AFARIKI DUNIA
Mchezaji wa zamani wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya Ghana Junior Agogo amefariki dunia jana jijini London akiwa na umri wa miaka 40.
Chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi, lakini inafahamika aliwahi kupata kiharusi mwaka 2015 ikiwa imepita miaka miwili tangu kustaafu kucheza soka.
Agogo ambaye aliichezea timu ya Taifa ya Ghana mechi 27, alikuwa katika kikosi cha timu cha Ghana kilichomaliza nafasi ya tatu katika michuano ya AFCON 2008.