KOMPANY AANZA KUPONDWA NA WACHAMBUZI
Mchezaji zamani wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Anderletch ya nchini humo Marc Degryse ameamua kumkosoa Vincent Kompany aliyejiunga na timu hiyo msimu huu 2019/20 kama kocha mchezaji baada ya kuondoka Man City.
Kompany amekoselewa vikali baada ya Anderletch kupata pointi mbili katika mechi nne za kwanza za ligi msimu huu, wakishika nafasi ya 13 kati ya timu 16 kufuatia kupoteza mechi mbili na kutoa sare mbili.
“Kompany ni mwanadamu, kando ya kuwa ni mwanasoka mzuri,ninahisi anafikiri yeye ni Mungu” alisema mshambuliaji wa zamani wa Anderletch Marc Degryse
“Yanapokuja mapumziko ya mechi za kimataifa kwa kawaida kocha huwa anakuwa na wiki mbili za kufanya kazi kiundani zaidi na kikosi chake lakini (Vincent) Kompany atakuwa na timu ya taifa (Ubelgiji) kwenda kucheza na San Marino na Scotland, kabla ya kucheza mechi ya kuagwa na Man City.
Kompany alipaswa afikirie kuhusu hili kuna mipaka katika kila kitu” alisema Marc Degryse kupitia HLN Sport
Kompany 33, anaifundisha timu hiyo huku akiichezea lakini bado hajastaafu kucheza timu ya taifa, kitu ambacho kinamfanya Marc Degryse aone Kompany anaweza asifanye vizuri.
Kompany alisababisha kuruhusu kufungwa baadhi ya magoli katika kipigo cha 4-2 walichopokea hivi karibuni kutoka kwa Kortrijk, na kupelekea Degryse kumtaka Kompany asijipange katika mchezo ujao kwa makosa hayo. Mechi ijayo Anderletch watacheza Ijumaa hii dhidi ya Genk ugenini.