STAA WA UGANDA THE CRANES KASAINI UTURUKI
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda na mpiga mipira ya adhabu ya timu hiyo Farouk Miya ,21, amepiga hatua kisoka baada ya kufanikiwa kupata timu mpya barani Ulaya.
Farouk ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Uganda The Cranes katika michuano ya AFCON 2019 nchini Misri, amefanikiwa kujiunga na klabu ya Konyaspor ya Ligi Kuu ya Uturuki akitokea timu ya Gorica ya nchini Croatia.
Ligi ya Uturuki inaonekana ni kubwa ukilinganisha na Ligi ya Croatia ndio maana inatajwa kuwa kapiga hatua.
Miya amesaini mkataba wa miaka mitatu na Kanyospor,msimu uliopita akiwa na Gorica alicheza michezo 30 na kufunga magoli 5.