Carvajal amwaga sifa kwa Lopetegui
Julen Lopetegui ametimuliwa kazi katika Real Madrid wiki iliyopita, lakini beki wa timu hiyo Dani Carvajal anasema kocha huyo ni bora zaidi.
Beki huyo wa kulia amesifu aina ya ufundishaji wa Lopetegui , akidai kuwa ni aina bora za ufundishaji kuwahi kufundishwa nazo.
“ Kwangu mimi, ni kocha bora kuwahi kuwa nae, “ beki huyo alisema katika mahojiano na kituo cha TVE cha nchini Hispania
“Bahati mbaya, alikosa bahati ndogo iliyohitajika ili kuendelea kuwa na sisi.
“ ( Ninapenda ) vile anavyouona mpira, jinsi anavyoongoza na vile anavyokaa na wachezaji “
“ Nilisema hili kabla hajaja Real Madrid na nitaendelea kusema hilo hata kama ameondoka.
Nitaendelea kusema hilo mpaka pale nitakapopata kocha mwingine anayefanya vizuri zaidi yake “
Carvajal alicheza mechi nane tu kipindi Julen Lopetegui akiwa kocha wa Real Madrid, akikosa mechi nyingi kufuatia kuwa majeruhi. Real Madrid sasa ipo chini ya kocha wa Team B Santiago Solari huku kocha wa kudumu akitafutwa.