HAZARD ANUNUA JUMBA LA BILLIONI 27 MADRID
Nyota mpya wa Real Madrid Eden Hazard amenunua nyumba ya kifahari jijini Madrid kwa Pauni Milioni 10 ambayo ni sawa na Tsh Bilioni 27.9
Nyumba hiyo ina vyumba sita vya kulala,mabafu 10, bwala la kuogelea,gym,spa,chumba cha cinema na uwanja wa tenesi.
Nyumba hiyo ya mchezaji huyo mwenye mke na watoto watatu wa kiume, ipo katika eneo ambalo wachezaji wengi wa Real Madrid wanaishi.