SANE KUFANYIWA UPASUAJI AUSTRIA
Wachezaji wa Man City jana wakati wa kupasha misuli kabla ya mechi dhidi ya Tottenham,walivaa jezi ya mchezaji mwenzao Leroy Sane ikiwa ni ishara ya kutoa pole na heshima kwa winga huyo aliyeumia goti lake la kulia katika mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Liverpool mapema mwezi huu.
Kocha wa Man City Pep Guardiola amesema kuwa Sane anataraji kwenda kufanyiwa upasuaji wa goti lake nchini Austria.
Mjerumani huyo,23,anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi saba akiuguza majeraha hayo.