ROGER FEDERER ATOLEWA NA ANDREY RUBLEV
Katika mashindano ya Cincinnati Masters, bingwa wa mashindano haya mara 7 Roger Federer ametolewa na kinda Andrey Rublev kwa seti mfululizo 6 – 3, 6 -4.
Ikiwa ni ushindi wake mkubwa Rublev aliyepo katika nafasi ya 70 hakusita elezea hisia zake juu ya gwiji huyu akisema “Naimani siku moja nitajihisi kama Roger. Kucheza na watu wote kukupa sapoti hadi mwisho.”
Federer aliyepo katika nafasi ya 3 kwa sasa anajipanga kushiriki michuano ya US Open mwezi huu na alimsifia Rublev kwa kumpa upinzani mkali na kusema amefurahishwa na mchezo aliocheza kinda huyo.