PHILIPPE COUTINHO AJIUNGA NA BAYERN MUNICH
Klabu ya Bayern Munich imetangaza kufikia makubaliano na Barcelona ya kumsajili kiungo mshambuliaji Philippe Coutinho kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja huku kukiwa na chaguo la kumnunua.
Mabingwa hao wa Ujerumani wamesema usajili huo unataraji kukamilikia katika siku chache zijazo.
Mbrazil huyo,27, ambaye alikuwa jukwaani jana wakati Barcelona inapoteza dhidi ya Athletic Bilbao, alijiunga na Wacatalunya hao Januari 2018 kwa ada ya Pauni Milioni 142 kutoka Liverpool.
Coutinho amefunga magoli 21 katika mechi 76 alizocheza Barcelona, lakini hiyo haijawashawishi wengi kufuatana na taraji kubwa kwake.