Real Madrid wapata dili kubwa kwa Adidas
Real Madrid wameripotiwa kukubali dili jipya la udhamini na kampuni ya vifaa ya michezo Adidas lenye thamani Euro Bilioni 1.1 (Pauni milioni 950) kwa mkataba wa miaka 10.
Hili litakuwa ni dili kubwa katika udhamini wa jezi kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu, wakiupiku mkataba wa miaka 10 wa Man United na Adidas waliosaini mwaka 2013 wenye thamani ya Pauni Milioni 750.
Kampuni hiyo itawalipa Los Blancos Euro Milioni 110 kwa mwaka, mara mbili ya Euro Milioni 52 wanazowalipa kwa mkataba wa sasa.
Adidas imekuwa ikiidhamini Real Madrid tangu mwaka 1998, awali walikuwa na mkataba na timu hiyo kati ya mwaka 1981 na 1986.