BARCA KUMKOSA MESSI UFUNGUZI WA LALIGA
Barcelona wamethibitisha Lionel Messi hatakuwepo katika kikosi chao cha leo kitakachocheza mechi ya ufunguzi wa msimu mpya wa LaLiga watakayocheza dhidi ya Athletic Bilbao katika dimba la San Memes.
Mfungaji huyo wa muda wote wa Barcelona anakosa mchezo huo kufuatia kuendelea kuuguza maumivu ya shavu lake la mguu aliyoyapata katika kipindi cha maandalizi ya msimu.