RIVALDO AMKINGIA KIFUA NEYMAR JR
Nyota wa zamani wa Barcelona Rivaldo amesema hafikirii kama Neymar akijiunga na Real Madrid itamfanya awe msaliti kwa timu yake ya zamani.
Neymar ambaye ameondoka Barcelona mwaka 2017 na kujiunga na PSG, anaripotiwa kutaka kuwahama matajiri hao wa Paris katika majira haya ya kiangazi na kuna uwezekano wa kurudi Barcelona au kwenda Real Madrid.
.
“Kama Zidane atamsajili Neymar Real Madrid, sitoona kama ni usaliti,” Rivaldo aliongea katika mahojiano na Betfair.
.
“Neymar aliondoka Barcelona na kusajiliwa na PSG,na sasa anaweza kwenda Real Madrid.
Hii si sawa kama angeondoka Barcelona na kwenda (moja kwa moja) Real Madrid.”