PEDRO ATOA UFAFANUZI KUHUSU RAMOS NA VAN DIJK
Nyota wa klabu ya Chelsea Pedro Rodriguez ametoa taarifa rasmi ya kufafanua kuhusiana na maoni yake aliyoitoa kabla ya mchezo wa UEFA Super Cup 2019 kuhusiana na kuwataja Virgil van Dijk wa Liverpool na Sergio Ramos wa Real Madrid kama mabeki bora duniani.
Vyombo vingi vya habari vimemnukuu vibaya kwa kudai kuwa Pedro amesema Dijk na Ramos ndio mabeki bora wa kati duniani, Jana kabla ya mchezo huo wa Uefa Super Cup, Pedro kupitia ukurasa wake wa facebook aliweka wazi kuwa katafsiriwa vibaya.
“Ninataka kuelezea kwa kila shabiki kuhusiana na press conference ya jana (juzi), sikusema kuwa Ramos na Van Dijk ndio mabeki bora wa kati duniani kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti”.
“Nilijibu swali nililoulizwa ni utofauti gani nauona kati yao (Ramos na Van Dijk), hivyo nilikuwa na zungumza kuhusiana na uwezo wao na nikasema wote ni wazuri”.
“Kama utaniuliza beki gani ni bora nichague mmoja kwa sasa nitasema ni Pique, ninafikiri ndio beki bora wa kati anayecheza kwa sasa.Beki bora wa kati niliyewahi kucheza nae ni Carles Puyol na ndiye ninayemkubali zaidiā