REDBULL WAMTEMA PIERRE
Siku chache baada ya boss wa Red Bull kudai bado timu hiyo inamuhitaji dereva Piere Gasly, timu hiyo sasa imetangaza kubadilishana dereva huyo na Alex Albon wa Toro Rosso. Sasa Pierre Gasly atajiunga na Toro Rosso kuendesha pamoja na Daniil Kvyat huku Alex Albon akiingia RedBull kuendesha pamoja na Max Vertapen.
Hatua hii imekuja baada ya Gasly kushindwa kufanya vyema baada ya kujikusanyia pointi 63 na kumuweka katika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa madereva ikilinganishwa na Max Verstapenn aliyejikusanyia pointi 182 na kuwa katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa madereva.
RedBull wanashindana kuwania nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa timu kwa sasa wakiwa katika nafasi ya 3 na pointi zao 244 nyuma ya Mercedes na Ferrari wenye point 438 na 288. Hivyo wanahitaji kuhakiki madereva wao wote wawili wanamaliza katika nafasi za juu ili kuweza kujikusanyia pointi nyingi na za kutosha kwa timu.