Yanga wameomba waambiwe moja Manji karudi au bado?
Mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa klabu ya Young Africans Kapten Mstaafu George Huruma Mkuchika amesema bado hajapokea barua kutoka kwa uongozi wa umoja wa matawi ya klabu hiyo, kuhusu ombi lao la kutaka aitishe mkutano mkuu wa dharura ambao utaweka wazi mustakabali wa uwepo ama kuondoka jumla kwa mwenyekiti Yusuph Manji.
Mkuchika amesema taarifa za uongozi wa matawi kumuomba aitishe mkutano mkuu wa dharura amekua akizisikia katika vyombo vya habari, lakini ameahidi endapo atapata barua hiyo atakaa chini na wajumbe wake na kujadili kwa kina na baadae watatoa majibu.
“Mimi na wajumbe wenzangu kazi yetu kusimamia mali ya Yanga uendeshaji wa kila siku hayo mengine mnayapata kwa mwenyekiti na kamati yake ya utendaji ila uendeshwaji wa klabu hatushughuliki baraza la wadhamini, sisi baraza la wadhamini tuna miliki mali za klabu ya Yanga, kwa hiyo uendeshaji wa klabu kila siku sijui nini na nini mwenyekiti sijui amerudi au hajarudi hayo unayapata kwa Katibu Mkuu na Msemaji wa Club”-Mkuchika
Hata hivyo Mkuchika ametoa angalizo kuhusu mchakato huo wa ombi la uongozi wa matawi ya Young Africans kwa kusema, baraza analoliongoza klabuni hapo linashughulika na mali za klabu na katua halijawahi kujihusisha na masuala ya utendaji na mambo mengine.