TYSON FURY VS OTTO WALLIN KUPIGWA SEPTEMBA 14 VEGAS
Baada ya pambano la Tyson Fury dhidi Otto Wallin kuthibitishwa kufanyika tarehe 14 Septemba katika ukumbi wa T-Mobile Arena, Las Vegas, bondia Msweden Otto Walllin amekiri kuwa ni ‘underdog’ katika pambano hilo.
“Ninajua mimi ndio ‘underdog’ katika pambano hili ila nimejiandaa kwa nafasi hii na nimeipokea kwa mikono miwili. Yeyote anaweza kupigwa hasa katika uzito wa juu .
(Katika pambano hili) nina vingi vya kuongeza na Fury ana kila kitu cha kupoteza.”
Otto mpaka sasa amepigana mapambano 20 na kushinda yote huku 13 yakiwa kwa KO japo hajawahi pambana na mabondia wa kaliba ya Fury.
Fury amepigana mapambano 29, akishinda 28, 20 yakiwa kwa KO, sare 1 dhidi ya Wilder na hajawahi kupoteza.
Fury anahitaji kushinda pambano hili ili kujiweka katika nafasi ya kurudiana na Wilder mapema mwaka 2020 huku Wilder akiwa na kibarua cha kupambana na Luis Ortiz wa Cuba mwishoni mwa mwaka ili kuhakiki nafasi ya kukutana na Furry.