LOUIS SAHA KATAJA SABABU ZA LUKAKU KUCHEMKA OLD TRAFFORD
Nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United Louis Saha kaeleza anachoamini kuwa ilikuwa sababu kuu ya nyota wa kibelgiji Romelu Lukaku kushindwa kufanya vizuri Manchester United. Saha 41, ambaye amewahi kuichezea Manchester United kwa miaka minne (2004-2008) amesema Lukaku ameshindwa kung’aa kwa sababu ya kukosa hamasa binafsi na kushindwa kujiamini.
“Lukaku hakuweza kuonesha uwezo wake Man United nafikiri ni kwa sababu ya kukosa hamasa mwenyewe na kupoteza kujiamini. Alikuwa kidogo hana bahati, Si aina ya mchezaji anayeweza kutengeneza goli na kufunga mwenyewe, anahitaji kuhudumiwa” alisema Saha katika mahojiano na Bwin
Lukaku alijiunga na Manchester United 2017 akitokea Everton kwa dau la pauni milioni 75 akiichezea Manchester United jumla ya michezo 96 ya mashindano yote na kufunga magoli 42 na sasa ameenda Inter Milan kwa uhamisho wa pauni milioni 74.