MARCELO HAJAWAHI KUFIKIRIA KUWA ATAVAA JEZI YA JUVENTUS
Beki wa Real Madrid Marcelo ,31, ameweka wazi kuwa alipokea ofa kutoka klabu za Ligi Kuu ya Italia lakini aliamua kuzipiga chini na kuendelea na maisha yake ndani ya Real Madrid licha ya kuanza katika mechi 21 tu za LaLiga msimu uliopita dhidi ya Sergio Reguilon.
Kabla ya ujio wa Zidane kama kocha wa Real Madrid kwa mara ya pili, chini ya utawala wa kocha Santiago Solari beki Marcelo alikuwa anaanza kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza.
Baada ya kuwa katika nafasi ngumu alianza kuhusishwa kujiunga na vilabu vya Italia ikiwemo Juventus kitu ambacho amekanusha vikali kuwa hawezi kujiunga nao, ana mapenzi na Real Madrid aliyojiunga nayo toka 2007 akitokea Fluminense ya kwao Brazil.
.
“Nilihitajiwa na klabu za Italia,lakini ukweli ni kwamba hizo zilikuwa ni tetesi tu naipenda Real Madrid ni nyumbani kwangu na klabu bora duniani, katika kichwa changu sijawahi kuwaza kama nitavaa jezi ya Juventus , nimejizatiti Real Madrid” alisema Marcelo akihojiwa na Gazzetta dello Sport