MOURINHO AMUITA ‘GENIUS’ AUBAMEYANG WA ARSENAL
Bao la dakika ya 58 la mshambuliaji wa Arsenal Pierre Aubameyang katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United linamuweka katika vitabu vya kumbukumbu za rekodi katika klabu hiyo.
Aubameyang baada ya kutupia bao hilo anakuwa kafikisha jumla ya mabao 33 katika mechi zake 50 za kwanza za ligi kuu nchini England, ambapo anakuwa kafunga magoli mengi zaidi katika idadi hiyo ya mechi katika historia ya Arsenal, akiwapiku Thierry Henry ,Ian Wright na Robin Van Persie.
Msimu uliopita Aubameyang aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu England kwa kufunga magoli 22 sawa na Sadio Mane na Mohammed Salah wa Liverpool, baada ya kufunga bao hilo na kiwango alichokionesha kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho ameonesha kukubali uwezo wake na kumuita ni genius.
.
“Anapenda kukaa mbele ya kipa, ni mtulivu….ninachopenda kusema ,mara nyingine (unaweza kumuita) Genius.
Hiyo control inaonekana kama rahisi lakini sio rahisi, ni genius” alisema Mourinho baada ya mchezo wakati akiongea katika kituo cha Sky Sports ambapo alikuwa ni mchambuzi.