POGBA KAWAAMBIA UKWELI MAN UNITED BAADA YA JAMBO LAKE KUSHINDWA KUTIMIA
[14:41, 8/11/2019] Traveller 1: Imeripotiwa kuwa nyota wa Manchester United n Paul Pogba amewatoa hofu viongozi wa timu hiyo kutokana na baadhi yao kuamini kuwa anaweza asiwe na mchango chanya msimu 2019/20 kwa kudhani akili yake imehama.
Pogba alikuwa anahusishwa kwa karibu kuwa katika mipango ya kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane na mwenyewe alishawahi kuripotiwa kuomba kuondoka ndani ya Man United lakini dili hilo lilishindwa kutimia katika majira haya ya joto.
Paul Pogba amewatoa hofu viongozi wake kuwa hawezi kuwa mfano mbaya katika timu na kushawishi vitu hasi kwa sababu tu jambo lake halijatimia na akili yake na fikra vitaendelea kuwaza kuitumikia Man United.
Inaaminika kuwa mchezaji akiomba kuondoka halafu uhamisho wake ukashindikana basi hawezi kucheza vizuri kwani atakuwa hana furaha na akili yake inaweza isiwe katika timu, hata hivyo kocha wa Man United Ole Gunnar Solkjaer anamtazama Pogba kama nahodha ajaye baada ya Ashley Young ambaye anaelekea kumaliza maisha yake ya soka Old Trafford.
SOURCE: Dailymail