NAOMI OSAKA AREJEA KILELENI HATA BAADA YA KUFUNGWA NA SERENA
Katika michuano ya Roger Cup, nyota Serena Williams amemfunga Naomi Osaka kwa seti 6-3, 6-4 na kufanikiwa songa katika hatua ya nusu fainali atakapokutana na Marie Bouzkova.
Hata baada ya kichapo hicho mchezaji Naomi Osaka amefanikiwa rejea kileleni katika msimamo wa wacheza Tennis kwa wanawake baada ya Karolina Pliskova aliyemtoa katika nafasi hiyo mwezi Juni kushindwa tetea nafasi hiyo baada ya kufungwa na Bianca Andreescu kwa seti 6-0, 2-6, 6-4.

Hii ni mara ya kwanza kwa Naomi Osaka kukutana na Serena tokea walipokutana katika fainali za US Open mwaka jana na Naomi kushinda taji lake la kwanza la Grand Slam.