REDBULL KUMBAKIZA PIERRE
Pamoja na dereva Pierre Gasly kutokuonyesha kiwango kizuri kilichotarajiwa na timu yake, Boss wa timu ya RedBull Christian Horner ameibuka na kudai bado wanamuhitaji dereva huyo.
Aliongeza na kusema “Ni muhimu kwetu kuwadaka Ferrari na kufanikiwa katika hilo tunahitaji Gasly afanikiwe kumaliza mbele zaidi sababu bila magari yote mawili kumaliza katika nafasi za juu inatuumiza.”

Pierre Gasly ameshindwa kuwa na msimu mzuri akiwa amejikusanyia pointi 63 huku nafasi nzuri aliyomaliza ikiwa ni nafasi ya nne ikilinganishwa na dereva mwenza Max Verstappen aliyejikusanyia pointi 181 hadi sasa na kumaliza katika nafasi ya kwanza mara mbili huku akiwa moja ya madereva wanaotoa upinzani mzuri kabisa kushindania nafasi tatu za juu.
Boss huyu wa RedBull hakuishia hapo kwani alikazia na kusema wataendelea fanya kazi ya kumpatia gari zuri ila anahitaji jipanga fanya vyema kwenye nusu ya msimu huu kwani hawatakiwi shindana na timu za Saubers na McLaren.
Kwa sasa timu ya RedBull inashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 244 nyuma ya vinara Mercedes wenye point 438 na Ferrari wenye pointi 288.