JE LIVERPOOL WANAWEZA ONDOA MKOSI WAO WA NAFASI YA PILI?
Msimu 2018/19 klabu ya Liverpool ilimaliza katika nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 97 na kuweka rekodi ya kuwa mshindi wa nafasi ya pili aliyejikusanyia pointi nyingi. Jumuisha na kushinda ubingwa wa Ulaya klabu hii imejiwekea ari ya kuwa mshindani wa kutwaa taji hilo msimu huu mpya wa 2019/20 baada ya hapo jana kuwakaribisha wageni Norwich City kwa kipigo cha goli 4 – 1 katika mechi ya kwanza ya ligi
Lakini hii si mara ya kwanza kwa klabu hii kumaliza katika nafasi ya pili kwani wameshamaliza katika nafasi hii misimu mingine minne na katika kila msimu uliofuata walipata anguko la kushindwa maliza hata katika nafasi nne za juu.

Misimu waliyomaliza katika nafasi ya pili ni 1990-91 kisha kumaliza nafasi ya 6 msimu uliofuata, 2001-02 na kumaliza nafasi ya 5 msimu uliofuata, 2008-09 na kumaliza nafasi ya 7 msimu uliofuata na 2013-14 na kumaliza nafasi ya 6 msimu uliofuata.
Msimu uliopita 2018-19 walimaliza nyuma ya Manchester City kwa point 1 hivyo swali ni wataweza vunja utaratibu wao wa kuporomoka msimu huu ulioanza?