Allison Becker kukosa mechi dhidi ya Chelsea UEFA Super Cup
Liverpool wamethibitisha kipa Allison Becker atakosa mechi ya UEFA Super Cup dhidi ya Chelsea Jumatano Ijayo Istanbul baada ya kuumia shavu la mguu katika mechi ya jana usiku dhidi ya Norwich.
Mbrazil huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo ili kujua atakaa nje ya uwanja kwa muda gani.