VAN DIJK: MAGUIRE ATAHITAJI KABILIANA NA PRESHA
Beki wa Liverpool Virgil Van Djik aliyekuwa akishikilia rekodi ya usajili wa bei ghali wa pauni 75 millioni kabla ya rekodi hiyo kuvunjwa na Harry Maguire aliuejiunga na Man United kwa pauni 80 millioni ameibuka na kudai rejodi hiyo huja na presha kubwa toka kwa mashabiki na wadau wa soka ila bado ingekuwepo tu kutokana na ukubwa wa klabu kama Manchester United.
“Unahitaji weka mawazo yako katika kile kitu unapenda kufanya na kucheza mpira mzuri. Cheza kwa kiwango chako bora kila uwapo uwanjani, furahia mpira na usiwaze chochote nje ya hapo.”
Aliongeza “Usiruhusu wapinzani watumie kigezo cha dau lako la usajili kama kigezo cha matokeo ya mechi. Huwa siwasikilizi sababu haitabadili chochote.”