Azam FC itarudi uwanjani November 22 2018.
Mara baada ya kumaliza mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar, kikosi cha Azam FC kinatarajia kucheza mchezo mwingine Novemba 22 mwaka huu dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Ligi kuu ya soka Tanzania bara itasimama kwa siku 18 kupisha michezo ya kufuzu Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon, ambapo Tanzania ‘Taifa Stars’ inatarajia kukipiga na Lesotho ugenini Novemba 18 mwaka huu.
Wachezaji wa Azam FC walioitwa kuunda kikosi cha timu hiyo ni mabeki Nahodha Agrey Moris, Abdallah Kheri, viungo Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mshambuliaji Yahya Zayd.
“Kikubwa tunamshukuru Mungu tumeweza kufanikisha lile lengo ambalo lilituleta, niwashukuru wachezaji na Staff kwa ujumla ushirikiano wetu umefanya tuweze kupata point tatu licha ya mazingira ya muda mgumu ambao sisi tulipangiwa kucheza saa nane kutokana na hali hewa hapa ilikuwa ni joto sana, Tunacheza na timu kama Kagera timu ambayo inakaa na watu tisa nyuma ya mpira kila wakati”-JUMA Mwambusi
Nyota wengine wa kimataifa wa Azam FC walioitwa timu za Taifa, ni beki Nickolas Wadada, aliyeitwa Uganda ‘The Cranes’ inayotarajia kucheza na Cape Verde pamoja na kiungo mshambuliaji Tafadzwa Kutinyu, aliyejumuishwa katika kikosi cha Zimbabwe.